Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

252 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

usalama, na utele. Katika Maandiko ya Agano la Kale upako huu maalum wa mafuta (kutiwa nguvu) wa Roho Mtakatifu kwa kawaida ulifanyika kwa wale tu waliohudumu kama manabii, makuhani, au wafalme. Katika Agano Jipya, kila mwamini katika Kristo, anapokea upako wa Roho Mtakatifu kuwa mhudumu wa uzima kwa wengine. (1) 1 Samweli 16:13a (linganisha na Isa. 61:1). (2) Luka 4:18 (3) 2 Wakorintho 1:21-22 (4) 1 Yohana 2:20 & 27 (linganisha na Yohana 14:26) c. Moto – Kinga ya Maisha (au utakaso wa Maisha). Ulimwengu wa zamani haukuwa na dawa za kuua vijidudu. Njia kuu ya kusafisha na kutakasa ilikuwa ni kutumia moto. Takataka zilichomwa ili zisiwe mahali ambapo vijidudu vya magonjwa vingezaliana (Law. 8:17). Ugonjwa ulipozuka, mara nyingi kuchoma nguo za mtu aliyeambukizwa ilikuwa njia pekee ya kuzuia ugonjwa huo usienee (Law. 13:47-59). Moto pia ulisafisha chuma na kuzifanya kuwa safi na bora kwa matumizi (Mal. 3:2-3). Katika Maandiko yote Mungu anatumia ishara ya moto kuzungumzia utakaso wa watu wake. Kwa mfano, nabii Isaya anazungumza kuhusu siku “Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza” (Isa. 4:4). (1) Mathayo 3:11-12 (2) Matendo 2:3-4 (3) 1 Wathesalonike 5:19 (4) Roho Mtakatifu kama moto wa Mungu, hulitakasa Kanisa daima, akililinda dhidi ya maambukizi ambayo dhambi inaweza kuleta.

Ibid . uk. 19.

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Ibid . uk. 40, 110.

d. Hua (njiwa) – Ishara ya maisha mapya Katika Mwanzo sura ya 8, wakati Mungu ameharibu uhai wote duniani kwa sababu ya dhambi, ni Nuhu tu, familia yake, na kundi la wanyama waliobaki

Ukurasa wa 132  9

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker