JINSI YA KUTAMBUA UHALIFU MISITUNI - AFRIKA- Swahili

Biashara haramu na unyonyaji katika flora, kama vile uvunaji haramu, imekuwa inakadiriwa kuwakilisha thamani ya 30-100,000,000,000 USD kwa mwaka.

A Centre Collaborating with UNEP

JINSI YA KUTAMBUA UHALIFU MISITUNI AFRIKA

1

2

JINSI YA KUTAMBUA UHALIFU MISITUNI AFRIKA

A Centre Collaborating with UNEP

3

Ni muhimu kufuatilia mbao katika mfululizo wote wa ugavi ili kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa katika kila hatua. KUTOKA MISITUNI HADI MADUKANI

Ian Redmond Reuters/Naco Doche/Scanpix

AKG-Images/Scanpix

HATUA 2

• Kupitia barabara kwa malori (shehena zinazoonekana waziwazi) • Kupitia njia za maji kwa mashua (shehena zinazoonekana waziwazi) • Kupitia njia za maji kwa kueleza mbao USAFIRISHAJI HADI VIWANDA VYA UPASUAJI WA MBAO

HATUA 1

• Eneo linalomilikiwa • Eneo linalohifadhiwa UVUNAJI

• Viwanda vya upasuaji wa mbao • Viwanda vya kusindika rojo ya mbao (kwa mfano vibanzi) • Viwanda vya karatasi UZALISHAJI

HATUA 3

4

Christian Nellemann

HATUA 4

• Kupitia mitandao ya barabara za kitaifa na kimataifa kwa malori (shehena iliyofungwa) • Kupitia njia za majini za kitaifa na kimataifa (shehena iliyofungwa) USAFIRISHAJI HADI MADUKANI

Wei Peiquan/Corbis/All Over Press

HATUA 5

• Soko za kitaifa • Soko za kimataifa MATUMIZI

5

UVUNAJI HARAMU

Christian Nellemann

Mfano wa kibali batili cha kukata miti.

UVUNAJI HARAMU TAMBUA

!

• Hakunaa kibali cha kukata miti • Kibali batili cha kukata miti (kibali kilichopitwa na wakati au bandia) • Kibali batili kwa ajili ya uvunaji, spishi na aina za usafarishaji • Uvunaji katika maeneo yasiyoruhusiwa

6

Peter Prokosch

Uvunaji ni haramu nyuma ya mabango ya mbuga za kitaifa.

AKG-Images/Scanpix

7

Toby Smith/EIA

Gogo la Mwaridi, mti unaoorodheshwa na CITES kama mojawapo ya spishi zilizo hatarini nchini Madagascar.

• Ukataji wa spishi zenye thamani ya juu na zilizoorodheshwa katika CITES (Mapatano ya Biashara ya Kimataifa ya Spishi za Wanyama na Mimea Pori zilizo Hatarini) • Hati batili (ikijumuisha kibali cha CITES) • Magogo haramu ya spishi zilizohifadhiwa, yanayojumuishwa katika ugavi wa tasnia ya rojo ya mbao. UVUNAJI HARAMU ! TAMBUA

Magogo ya Afrormosia, mti unaoorodheshwa na CITES kama mojawapo ya spishi zilizo hatarini nchini Kongo.

8

AFP Photo/Jiro Ose/Scanpix

9

KILIMO NA MIGUNDA INACHUKUA MAHALI MISITUNI

Prill Mediendesign & Fotografie/iStock

Misitu huondoshwa ili kutoa nafasi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashara na kuanzisha na kupanua migunda ya mawese.

10

Apichat Naweewong/iStock

Eneo la kilimo karibu na mpaka wa msitu usiopenyeka wa Bwindi nchini Uganda.

• Misitu iliyoondoshwa kwa ajili ya mazao ya biashara kwa kutumia vibali batili • Misitu iliyomo mbuga za kitaifa au maeneo yanayomilikiwa isivyo halali, inayoondoshwa kwa ajili ya kilimo UKATAJI MITI HARAMU ! GUNDUA

11

UZALISHAJI WA MKAA Kusimamia uzalishaji na biashara ya mkaa ni muhimu sana hasa barani Afrika. Uzalishaji wa mkaa huenda ukatekelezwa kwa njia ya haramu, na mapato kutoka kwa biashara hii huenda ya katumiwa kusaidia shughuli za kihalifu barani Afrika.

Christian Nellemann

Malori yaliyopakiwa mkaa nchini Uganda.

Mkaa yakiwa tayari kusafirishwa nchini Uganda.

12

GUNDUA

!

• Tanuru za kuchomea mkaa katika mbuga za kitaifa. UKATAJI MITI HARAMU

Christian Nellemann

13

USAFIRISHAJI HADI VIWANDA VYA UPASUAJI WA MBAO

Ian Redmond

Ian Redmond

Usafirishaji wa magogo kwa malori.

Usafirishaji wa magogo kwa njia za maji.

GUNDUA

!

MAGOGO HARAMU KATIKA NJIA ZA USAFIRISHAJI

• Hakuna kibali cha usafirishaji • Kurudia matumizi ya kibali kilekile • Kupita maeneo ya ukaguzi bila kibali

14

Spishi zinazohifadhiwa na kukatwa kwa njia haramu zinaweza kuwepo katika maghala ya viwanda vya upasuaji wa mbao. UTENGENEZAJI

Reuters/Naco Doche/Scanpix

Mfanyikazi apasua mbao zilizokatwa kiharamu.

TAMBUA

!

MAGOGO HARAMU

• Mbao zenye ukubwa wa kupindukia katika viwanda vya kupasua mbao au katika maeneo mengine ya utengenezaji • Mbao za spishi zinazohifadhiwa (labda mbao zenye uzito mkubwa) katika viwanda vya upasuaji mbao au maeneo mengine ya utengenezaji. • Akiba kubwa sana ya mbao katika viwanda vya upasuaji wa mbao au maeneo mengine ya utengenezaji • Kushindwa kuweka kibonyeo katika mbao kwa chombo chenye makali. Ikiwa ni mbao yenye uzito mkubwa, kuna uwezekano kwamba ni mbao iliyotoka kwa mti wa zamani wa msitu wa mvua.

15

USAFIRISHAJI HADI MADUKANI

Christian Nellemann

Corbis/All Over Press

Mbao zinazoelea karibu na bandari ya Libreville nchini Gabon.

Mbao zikisafirishwa kwa malori,

• Usafirishaji wa mbao usioripotiwa kikamilifu kwa vyombo majini na/au kwa malori barabarani • Kufanya magendo kutumia vibali bandia USAFIRISHAJI HARAMU ! GUNDUA

16

Makambi ya wakataji miti hutegemea“nyama ya porini”kutoka kwa wanyama walio hatarini kama vile sokwe na sokwe-mtu. Zaidi ya hao, wakataji miti huenda wakajihusisha na biashara ya pembe za ndovu na vifaru. UJANGILI WA WANYAMA WA PORINI

Corbis/All Over Press

Vichwa na mikono ya sokwe vikiuzwa.

Sokwe-mtu wako hatarini kwa sababu ya kupotea kwa makao na uwindaji haramu.

Science Photo Library/Scanpix

17

AP Photo/STR/Scanpix

Pembe haramu za ndovu zilizokamatwa na maafisa wa bandari ya Mombasa nchini Kenya.

• Uwindaji haramu wa spishi za wanyama zilizo hatarini kama ilivyoorodheshwa na Mapatano ya Biashara ya Kimataifa ya Spishi za Wanyama na Mimea Pori zilizo Hatarini (CITES) • Biashara haramu ya pembe za ndovu UWINDAJI HARAMU WA WANYAMA WA PORINI ! GUNDUA

18

1. Zingira sehemu ya nje ya eneo la uhalifu ili wewe na wenzako mlisiliathiri. Egesha magari umbali wa angalau mita 100. Usisogeze chochote. KUENDESHA MASHTAKA DHIDI YA MSHUKIWA BAADA YA KUMKAMATA 3. Tayarisha mchoro sahili wa eneo la uhalifu, ukionyesha mahali halisi au uhusiano kati ya vitu vilivyomo na ushahidi. 4. Rekodi nyayo zozote, viatu au ishara zozote zinazodhibitisha kilichofanyika AU zinazomhusianisha mshukiwa na eneo hilo la uhalifu. 5. Kamata au kusanya kitu chochote ambacho unadhani kinahusiana na eneo la uhalifu, ikiwezekana kwa kutumia penseli, glavu au kijiti. Weka vitu katika mifuko tofauti tofauti au kwenye karatasi iliyokunjwa. 6. Tayarisha ripoti fupi au andika maneno makuu ukiwa katika eneo la uhalifu na jumuisha kitu chochote kinachoweza kuhesabiwa, kwa mfano, alama za nyayo, vitu vilivyokamatwa (silaha, risasi, vifaa vya kukatia, vipande vya wanyama wa porini, mifuko ya mkaa au magogo), na watu walioko -- pamoja na tarehe, saa, na muda uliokadiriwa kupita tangu tendo la kihalifu lilipotokea, muda uliotumia katika eneo la uhalifu, maelezo kuhusu eneo hilo na/au alama ambatanifu za kijiografia (coordinates). Hakikisha kwamba habari zinazokusanywa zitatosha kulipata eneo hilo tena. 2. Piga picha.

19

JINSI YA KUTAMBUA UHALIFU MISITUNI AFRIKA

ISBN: 978-82-7701-144-8

GRID-Arendal P.O. Box 183 N-4802 Arendal Norway

+47 4764 4555 grid@grida.no www.grida.no

INTERPOL General Secretariat Environmental Security Sub-Directorate 200 quai Charles de Gaulle 69006 Lyon, France environmentalcrime@interpol.int

Corbis/All Over Press

20

Made with