JINSI YA KUTAMBUA UHALIFU MISITUNI - AFRIKA- Swahili - page 19

19
1. Zingira sehemu ya nje ya eneo la uhalifu ili wewe na wenzako mlisiliathiri.
Egesha magari umbali wa angalau mita 100. Usisogeze chochote.
2. Piga picha.
3. Tayarisha mchoro sahili wa eneo la uhalifu, ukionyesha mahali halisi au
uhusiano kati ya vitu vilivyomo na ushahidi.
4. Rekodi nyayo zozote, viatu au ishara zozote zinazodhibitisha kilichofanyika AU
zinazomhusianisha mshukiwa na eneo hilo la uhalifu.
5. Kamata au kusanya kitu chochote ambacho unadhani kinahusiana na eneo la
uhalifu, ikiwezekana kwa kutumia penseli, glavu au kijiti. Weka vitu katika mifuko
tofauti tofauti au kwenye karatasi iliyokunjwa.
6. Tayarisha ripoti fupi au andika maneno makuu ukiwa katika eneo la uhalifu na
jumuisha kitu chochote kinachoweza kuhesabiwa, kwa mfano, alama za nyayo,
vitu vilivyokamatwa (silaha, risasi, vifaa vya kukatia, vipande vya wanyama wa
porini, mifuko ya mkaa au magogo), na watu walioko -- pamoja na tarehe, saa,
na muda uliokadiriwa kupita tangu tendo la kihalifu lilipotokea, muda uliotumia
katika eneo la uhalifu, maelezo kuhusu eneo hilo na/au alama ambatanifu za
kijiografia (coordinates). Hakikisha kwamba habari zinazokusanywa zitatosha
kulipata eneo hilo tena.
KUENDESHA MASHTAKA
DHIDI YA MSHUKIWA
BAADA YA KUMKAMATA
1...,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18 20
Powered by FlippingBook